Baada ya Pochettino kukabidhiwa kikosi cha mabingwa wa soka nchini Ufaransa PSG – meneja huyo kutoka nchini Argentina anahitaji kumbakiza mshambuliaji Moise Kean kwa mkataba wa moja kwa moja.

 Kean alijiunga na PSG kwa mkataba wa mkopo mwanzoni mwa msimu huu, akitokea Everton ya England.

Sambamba na Kean, habari nyingine zinaeleza kuwa Pochettino amewasiliana na nyota wa Tottenham Delle Alli, ili kufanikisha lengo la kumpeleka PSG.

  • Taarifa nyingine za USAJILI zinaeleza kuwa: Manchester United hawana mpango wa kumbakiza Amad Diallo katika klabu ya Atalanta na badala yake wanamuhitaji mchezaji huyo kujiunga na wenzake pale Old Trafford mwezi huu.

Sanjari na hayo, meneja Ole Gunnar Solskjaer atafanya mazungumzo na wachezaji takribani 6 kuhusu mipango yake na wachezaji hao, Japokuwa inavyoonekana, wachezaji hao wanaweza kutolewa kwa mkopo au kuuzwa moja kwa moja.

  • Hali si shwari pale Stamford Bridge, kibarua cha Frank Lampard kipo mashakani, na inasemakana uongozi wa klabu hiyo umeanza kuangalia mpango mbadala.
  • Mikel Arteta anatarajia kufanya mazungumzo na Alexander Lacazette kuhusu hatma ya mchezaji huyo klabuni hapo. Vilevile, Arteta anapanga kukatisha usajili wa mkopo wa Lucas Torreira na kumrudisha Emirate.
  • Beki Lucas Digne yupo mbioni kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia klabu ya Everton.
  • Mamlaka zinazosimamia soka nchini Uingereza zimeelekezwa kuwaadhibu wachezaji wanaokiuka utaratibu wa kujilinda na COVID19.

CAF waridhia ombi la Simba SC
Katibu Mkuu UN akemea utaifa chanjo ya Covid 19