Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma amekitaka Chama Cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kuacha uanaharakati na badala yake kisimamie misingi na kanuni za taaluma yao ikiwamo kuishauri serikali, mahakama na bunge.

Ameyasema jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uhalali wa chama hicho kwamba ni taasisi ya umma kutokana na kupewa jukumu la kuishauri serikali kuhusu masuala ya kisheria.

Aidha, amekitaka chama hicho cha wanasheria kuacha kulumbana kupitia vyombo vya habari kwasababu ni taasisi iliyoanzishwa kisheria lakini imepewa majukumu ya kufanyakazi ya umma.

“Niwashauri viongozi wapya wa TLS waache uanaharakati na kwamba wanatakiwa kushirikiana na mahakama katika masuala ya kisheria,”amesema Prof. Juma

Hata hivyo, amekitaka chama hicho kitimize majukumu ya umma ikiwamo kuisaidia serikali, makama na bunge nchini.

 

Mtoto wa miaka miwili auawa kinyama
Aslay agoma kushindanishwa na wasanii wenzake

Comments

comments