Hatimaye Uongozi wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC, umeitaja TP Mazembe kuwa mpinzani wa kikosi chao katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki utakaochezwa kwenye Tamasha la Siku ya Simba (Simba Day).

Tamasha la Simba Day ambalo huambatana na burudani mbalimbali, kwa mwaka huu 2019 limepangwa kufanyika, Septemba 19 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Simba SC wameitaja TP Mazembe kupitia utaratibu wao wa kutoa taarifa kwa njia ya mtandao (Simba App) usiku wa kuamkia leo Jumanne (Septemba 07), na kuzima tetesi zilizokuwa zinazunguzwa katika vijiwe vya soka, kuhusu timu ambayo ingecheza na Mabingwa hao wa Tanzania bara.

Awali Mabingwa wa Soka Barani Afrika klabu ya Al Ahly walikua wanatajwa huenda wangekuja nchini kucheza na kikosi cha Simba SC, na ungetumika kama sehemu ya kumuaga Luis Miquissone.

Kwa sasa Kikosi cha Simba SC imeweka kambi jijini Arusha kikiwa na mastaa kama Bernard Morrison, Chris Mugalu, Beno Kakolanya, Gadiel Michael, Henock Inonga na Pascal Wawa.

Ratiba ya FIFA yaivurugia Azam FC
Taifa Stars kusaka alama tatu leo