Kamishna wa Kodi za Ndani kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Elijah Mwandumbya amwataka wafanyabiashara kuacha kutoa sababu za ubovu wa mashine za kutolea risiti za kielektroniki (EFD) kwani mashine hizo sasa zinafanyakazi vizuri.
 
Ameyasema hayo alipokuwa akifanya ukaguzi wa kushtukiza katika maduka yaliyopo eneo la Mlimani city jijini Dar es Salaam.
 
Mwandumbya amesema kuwa wafanyabiashara wote wanaostahili kutoa risiti za EFD wanapaswa kutoa kwa kila mauzo wanayofanya kwani tatizo la mashine lilishashughulikiwa na limekwisha.
 
“TRA haitakubali mfanyabishara anayeonyesha barua kama sababu ya kutokutoa risiti ya EFD, tatizo la mashine lilikwisha, ni wajibu wa wafanyabiashara kutoa risiti”, amesema Mwandumbya.
 
Aidha, kwa upande wake Meneja wa duka la Woolworth lililopo Mlimani city, Joehans Mgimba amesema kuwa kwa sasa mashine za EFD hazina shida yoyote na kuwataka wafanyabiashara wengine kutoa risiti na mwisho kulipa kodi kwa maendeleo ya taifa.
 
Hata hivyo, TRA inaendelea kufanya ukaguzi wa matumizi ya mashine za EFD katika maduka mbalimbali yaliyopo mlimani city kwa Lengo la kuhakikisha kuwa kila mfanyabiashara anatoa risiti za EFD na kulipa kodi stahiki kwa mujibu wa sheria za kodi za nchi.
 
  • Picha: Miss Ilala, Dar24 Media wafanya ziara mashuleni
  • DC Mofuga asimamia zoezi la kuteketezwa kwa moto nyumba sita
  • Dkt. Kigwangalla awawashia moto waliovamia Pori la Akiba

Video: Nawasha moto wa kumchoma Mbowe, CCM inakotupeleka siko
Korea Kaskazini yaunda makombora mapya