Rais Donald Trump wa Marekani amebadili msimamo wake siku ya Jumatano na kutia saini amri ya utendaji inayositisha hatua ya kuzitenganisha familia na watoto wao wanapoingia Marekani kinyume cha sheria kwenye mpaka na Marekani na Mexico.

Ambapo sheria hiyo inahusu kuweka familia pamoja, wakati huo ikihakikisha kwamba kuna usalama thabiti wa mpaka huku sheria zikiendelea kuwepo kama ilivyokuwa hapo awali na kuimarishwa zaidi.

Hata hivyo amesisitiza kwamba amri hiyo haitobadili sera yake ya kutowastahimilia wahamiaji wanaojaribu kuingia Marekani kinyume cha Sheria.

“Sikupenda kile nilichokua nakiona pale familia zikitaabika wanapotenganishwa. Ni tatizo ambalo limekua likiendelea kwa miaka mingi kama mnavyofahamu kupitia utawala mbali mbali, na sisi tunafanya kazi kuleta mabadilkiko katika mfumo wa uhamiaji” amesema Trump.

Wachambuzi wa masuala ya siasa wanasema kuna mambo kadhaa yaliyomsababisha kuchukua hatua hiyo likiwemo shinikizo kutoka kwa mke wake Melania Trump ambaye mapema wiki hii kupitia msemaji wake alisema haungi mkono zoezi la kuwatenganisha watoto na wazazi wao.

Leo Bunge linatarajiwa kuipigia kura miswada miwili ambayo inalenga kuondoa utata huo wa kuziumiza familia na mapendekezo mengine ya masuala ya uhamiaji.

Hata hivyo mbali na Milania wake wa Marais wa zamani, Michelle Obama, Hillary Clinton na Laura Bush pamoja na viongozi wa dini  nao walikuwa hawaungi mkono matamshi hayo ya kuwatenganisha watoto na wazazi wao.

Aidha, Wizara ya Usalama wa Ndani itazishikilia pamoja familia za kigeni zilizoingia huku utaratibu wao wa kisheria kuhusu kuingia kiunyume cha sheria ukishughulikiwa.

 

Serikali yafaidika bilioni 1.5 gawio la TTCL
JPM awapa neema TTCL, aruhusu kupandisha mishahara