Rais Donald Trump wa Marekani amekubali ombi la Kiongozi wa Korea kaskazini, Kim Jong Un la kutaka wakutane mapema ndani ya mwezi mei mwaka huu.

Hatua hiyo inaweka historia kubwa kwa Marekani kwani haijawahi kutokea rais yeyote wa Marekani kukutana na kiongozi wa Korea Kaskazini.

Hayo yamesemwa ujumbe wa Korea Kusini ambao ulikutana na Rais wa Korea Kaskazini kwa ajili ya kufanya mazungumzo na rais huyo.

Aidha, rais Kim pia amekubali kusitisha mpango wake wa nyuklia na majaribio yake makombora, msimamo ambao ni tofauti na aliokuwa nao mwanzoni.

Hata hivyo, hatua hiyo iliyofikiwa ya rais Kim Jong Un ya kulegeza msimamo ni matokeo ya mazungumzo mazito yaliyofanywa wiki chache zilizopita na ujumbe wa Korea Kusini kukutana na kiongozi huyo.

Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Machi 9, 2018
Aliyefanyiwa upasuaji wa ubongo kimakosa azungumza