Zikiwa zimebaki siku kumi kabla ya timu ya Taifa soka la wanawake Twiga Stars kuikablri timu ya wanawake kutoka nchini Zimbabwe mchezo utakopigwa March 4 mwaka huu, timu ya Twiga Stars imeendelea kujifua vilivyo katika uwanja wa Karume uliopo jijini Dar es salaam chini ya kocha wao mpya Nasra Juma.

Akizungumzia kikosi chake Kocha Nasra, amesema hali ya kikosi chake kwa sasa ni nzuri na wachezaji wote wana morali ya hali ya juu dhidi ya wapinzani wao, na amefanya mchujo na kupata kikosi cha wachezaji 11 watakaoanza dhidi ya wazimbabwe March 4.

Nasra amesema kwa sasa hajapata mchezaji yeyote ambaye ni majeruhi na anaimani na kikosi chake kitafanya vizuri katika mchezo huo kutokana na uzoefu wa wachezaji wake ambao wameshazoea mikiki mikiki ya michezo ya kimataifa.

Kikosi cha Twiga Stars kimeweka kambi katika hostel za shirikisho la soka nchini TFF, zilizopo karume jijini Dar es salaam.

Kenya Watembelea Nyota Ya Soka La Bongo
Yanga Waendelea Na Maandalizi Dhidi Ya JKT Mlale