Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, leo novemba 29,2021 inaendelea na usikilizaji wa kesi ya Uhujumu uchumi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu, wanaotuhumiwa kwa makosa ya ugaidi.

Kesi hiyo iko katika hatua ya usikilizwaji wa kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi, inayohusu uhalali wa maelezo yanayodaiwa kuwa yalitolewa na mshtakiwa wa tatu, Mohamed Abdillahi Ling’wenya.

Mshtakiwa huyo wa tatu ambaye ni shahidi wa kwanza wa utetezi katika kesi hiyo ndogo leo anatarajiwa kumalizia ushahidi wake aliouanza tangu Ijumaa iliyopita, baada ya upande wa mashtaka kufunga ushahidi wake.

Mahakama hiyo inatarajiwa kutoa uamuzi wa pingamizi la upande wa mashtaka kuhusu barua ambayo mshtakiwa huyo anaiomba mahakama hiyo iipokee kama kielelezo cha ushahidi wa upande wa utetezi.

Barua hiyo ambayo Ling’wenya amemwandikia Kamanda wa Polisi Mkoa Ilala akiomba baadhi ya nyaraka za kuthibitisha maelezo ya ushahidi shahidii wa upande wa mashtaka katika kesi hiyo ndogo, kuwa mwaka 2020 alikuwa akifanya kazi kituo Kikuu cha Polisi Dar. (Central) na kwamba aliwapokewa yeye ( Ling’wenya) na mwenzake kitioni hapo na kuwahifadhi mahabusu.

Upande wa mashtaka ulipinga barua hiyo kupokewa kwa madai kuwa shahidi huyo (mshtakiwa) na kielelezo hicho hawajakidhi vigezo vya kupokelewa kuwa kielelezo.

Mbowe na wenzake wanakabiliwa na kesi ya uhujumu Uchumi namba 16/2021 yenye mashtaka sita yakiwemo ya kula njama na kufadhili vitendo vya kigaidi, vinavyodaiwa kuwa vikilenga kuleta hofu katika jamii ya Wananchi wa Tanzania

Wizkid na Chris Brown wafanya Kufuru O2 Arena London.
Rais Ramaphosa atoa wito kwa Nchi za Ulaya na Marekani kuondoa vikwazo