Miss Tanzania 2006, Wema Isaack Sepetu leo hii amehukumiwa kifungo cha jela mwaka mmoja au kutoa faini ya shilingi milioni mbili mara baada ya kukutwa na makosa mawili.

Kosa la kwanza likiwa ni kutumia dawa za kulevya aina ya bangi pisi tatu na kosa la pili ni kukutwa na madawa hayo nyumbani kwake.

Anbapo shahidi upande wa mashtaka ameieleza mahakama kuwa Bangi aliyokutwa nayo Wema kwenye mkojo ilikuwa imetumiwa ndani ya siku 28.

Hukumu hiyo imetolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mara baada ya kuhairishwa mnamo Julai 16, 2018 kutokana na sababu za kiuchunguzi ambazo Hakimu alikuwa anazifanyia kazi .

Aidha mnamo April 23, 2018 Wema Sepetu na wafanyakazi wake wawili walikutwa na kesi ya kujibu katika Mahakama hiyo kutokana na kukabiliwa na kesi ya kumiliki na kutumia dawa za kulevya aina ya bangi.

 

Neymar Jr aikataa Real Madrid
Ray C ampongeza Muna...'good job'

Comments

comments