Uchumi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar unazidi kukua kwa kasi kubwa kutokana na usimamizi mzuri uliopo katika ukusanyaji mapato, unaotokana na usimamizi mzuri wa sera nzuri za kiuchumi unaoendana na matakwa ya sasa kuelekea katika falsafa ya Zanzibar ya Viwanda.

Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt. Abdallah Juma Sadalla katika mahojiano maalumu kuhusiana na masuala ya kiuchumi.

Amesema kuwa wananchi wanatakiwa kutumia vizuri fursa na mazingira bora ya miundombinu iliyowekwa na Serikali kwa kufanya kazi kwa bidii hasa zile za uzalishaji mali ili waweze kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi.

Aidha, amewataka Wananchi kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Marais wa pande zote mbili ambao ni Rais wa Zanzibar ,  Dkt. Ali Mohamed Shein  pamoja na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, kwa kasi zao nzuri za kiutendaji juu ya maendeleo ya nchi.

Hata hivyo, ameongeza kuwa Zanzibar  imepata neema kubwa ya Uchimbaji na utafutaji wa rasilimali za Mafuta na Gesi Asilia ambazo kwa sasa tayari zimeanza kwa nchi nzima, hivyo amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwani fursa hiyo ni moja ya vitega uchumi muhimu vya kitaifa.

Video: Majaliwa awataka Mabalozi kutangaza fursa za uwekezaji Tanzania
Ujenzi wa Kingo za Bahari washika kasi Jijini Dar