Serikali ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (DARUSO) kupitia Wizara ya Afya imesema kuwa imopokea kwa masikitiko taarifa ya ajali iliyotokea June 11, 2018 maeneo ya Riverside Ubungo Jijini Dar es salaam.

Ajali hiyo imehusisha Ambulance ya Chuo na Hiace iliyokuwa na wanafunzi ambao wametambulika kwa majina ya, Soko Maria Godian aliyekuwa anasoma mwaka wa kwanza, Steven .E. Sango aliyekuwa anasoma mwaka wa pili, James ambaye alikuwa dereva wa Ambulance.

Hata hivyo, taarifa hiyo ya DARUSO imeeleza kuwa mwanafunzi mwingine Abishai Nkiko aliyekuwa anasoma mwaka wa tatu bado anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na hali yake bado ni mbaya zaidi.

Video: Bunge kumhoji mwanamke aliyejifungulia kituo cha polisi, Kiama viongozi wa umma J'tatu
Urusi 2018: Nani atabeba Kombe? Tuimulike Uingereza (England)

Comments

comments