Washambuliaji Gareth Bale na Cristiano Ronaldo wamekua miongoni mwa wachezaji walioteuliwa kwenye orodha ya wachezaji 10, wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa barani Ulaya msimu wa 2015-16.

Orodha hiyo imetolewa mapema hii leo na shirikisho la soka barani Ulaya UEFA, baada ya kamati maalum iliyowajumuisha waandishi wa habari kufanya kazi yake na kutoka na majima kumi ya mwisho.

Katika orodha hiyo, jina la mshambuliaji Ronaldo linaonekana kupewa uzito mkubwa kutokana na mafanikio aliyoyapata hivi karibuni ya kukiongoza kikosi cha timu ya taifa ya Ureno kutwaa ubingwa wa Euro 2016, pamoja na kuwa sehemu ya kikosi cha klabu ya Real Madrid ambacho kilitwaa taji ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Mshambuliaji mwenzake wa klabu ya Real Madrid, Garteh Bale naye anachagizwa na mafanikio ya kuisaidia timu yake ya taifa ya Wales kufika hatua ya nusu fainali ya Euro 2016.

Mwingine ambaye anatajwa kutoa upinzani katika harakati za kuwatwaa tuzo ya mchezaji bora wa msimu, ni mshambuliaji kutoka nchini Ufaransa na klabu ya Atletico Madrid Antoine Griezmann.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25, alimaliza michuano ya Euro 2016 akiwa mfungaji bora baada ya kufunga mabao sita.

Orodha kamili ya wachezaji kumi iliyotajwa na UEFA.

  1. Gareth Bale (Real Madrid & Wales)
  2. Gianluigi Buffon (Juventus & Italy)
  3. Antoine Griezmann (Atletico Madrid & France)
  4. Toni Kroos (Real Madrid & Germany)
  5. Lionel Messi (Barcelona & Argentina)
  6. Thomas Muller (Bayern Munich & Germany)
  7. Manuel Neuer (Bayern Munich & Germany)
  8. Pepe (Real Madrid & Portugal)
  9. Cristiano Ronaldo (Real Madrid & Portugal)
  10. Luis Suarez (Barcelona & Uruguay)

Mbeya City FC Yamnasa Rajab Zahir
Waziri Mkuu Kuwa Mgeni Rasmi Kongamano la uwekezaji.