Timu ya Taifa ya Ujerumani imeitupa nje Timu ya Taifa ya Uingereza katika michuano ya mpira wa miguu ya vijana barani Ulaya chini ya umri wa miaka 21.

Aidha, katika mchezo huo uliokuwa mkali na wa kusisimua Uingereza ilikuwa ya kwanza kupata goli katika dakika ya 41 kupitia kwa Demarai Gray huku Ujerumani ikisawazisha kupitia kwa Davie Selke.

Kipindi cha pili kiliendelea kwa timu zote mbili kushambuliana huku kila upande ukihitaji kupata goli ambalo litaiwezesha kusonga mbele katika michuano hiyo.

Hata hivyo, Ujerumani ilifanikiwa kuitungua Uingereza kwa penati 4-3 mara baada ya kutoka sare hali ambayo ilipelekea kufikia katika hatua ya matuta.

 

Valere Germain Apata Kiota Kipya Ufaransa
Odinga apiga marufuku ngono siku ya uchaguzi