Mkuu wa Idara ya Habari ya Klabu Bingwa Tanzania Bara Simba SC, Haji Manara ameonesha furaha ya ubingwa kwa kuandika maneno mazito kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Manara ameonesha furaha hiyo, huku zikisalia saa kadhaa kabla ya Nahodha na Mshambualiaji John Bocco hajakabidhiwa Kombe la ubingwa, baada ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Namungo FC utakaochezwa kesho Jumapili (Julai 18) Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Manara ameandika: “Kikombe kinaashiria ushindi, na ushindi hukupa furaha ya moyo wako”

“Usifadhaike na waliokuchafua jana na leo hata kesho, baki na furaha yako ya ushindi”

“Dunia ipo kwa ajili ya furaha, nimechafuliwa mangapi? Natukanwa mara ngapi? Mara ngapi nishasemwa?”

“Sijapungukiwa kitu na hawatakupungizia kitu,, ishi kwa amani na furaha hata kwa wanaokuchukia na kukuchafua kisha samehe, halafu endelea kuwaombea Dua, ipo siku Mungu atawazindua”

“Ujumbe huu ni kwa wote wanaochafuliwa na walimwengu, baki na furaha yako”

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Julai 18, 2021
Ninja atia neno fainali kombe la Shirikisho (ASFC).