Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Samia Suluhu Hassan ameuomba Umoja wa Mataifa kuondoa hati miliki kwenye uzalishaji wa chanjo ya Uviko-19 ili mataifa mengi yaweze kuizalisha na kuitoa kwa wananchi wake.

Amesema hayo wakati akihutubia mkutano mkuu wa baraza la UN huku akiutaka Umoja huo wa Kimataifa kuongeza ushirikiano wa kuyakabili majanga ya kimataifa.

“Ombi letu ni kwamba hati miliki ya kutengeneza chanjo ya Uviko-19 itolewe kwa nchi zinazoendelea ili tuweze kupambana na janga hili hatari, hii sio tu hatua ya muhimu ya kumaliza janga hili lakini pia ni jambo sahihi litakalosaidia kuokoa ulimwengu mzima.


“Wakati chanjo ya Uviko-19 ilipokuwa ikifanyiwa utafiti ulimwenguni na baadaye kutengenezwa wengi tulikuwa na matumaini kwamba hii itakuwa na maana kubwa kwetu sote, tumekuja kugundua kwamba kirusi hiki kinasambaa haraka zaidi kuliko utengenezwaji na usambazaji wa chanjo,” amesema Rais Samia.


Rais Samia amesema kuwa kulingana na kasi ya utengenezaji na usambazaji wa chanjo ya Uviko-19 kuwa ndogo ikilinganishwa na kasi ya usambaaji wa ugonjwa huo ni wazi kwamba itakua ngumu kufikia malengo yaliyowekwa na Shirika la Afya Dunia (WHO).

Watatu wakamatwa kwa utekaji nyara
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Septemba 24, 2021