Kada wa CCM, January Makamba ametoa taarifa njema kwa watanzania hivi punde kuwa chopa zote za chama hicho ziko salama na tayari ameongea na kila aliyedaiwa kuwa kwenye chopa iliyoripotiwa kuwa imepinduka na kuripuka.

“Updates: Taarifa Kuhusu Chopa Ya CCM Iliyolipuka Na Wahanga Wa Ajali Hiyo,” ametweet January Makamba.

 


Tangu jana kulikuwa na taarifa za kuanguka na kulipuka kwa chopa ya CCM ilyokuwa imewabeba makada wa chama hicho akiwemo mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe, katika eneo la Msolwa, hifadhi ya Selous.

Taarifa hizo ziliaminika na wengi kuwa za kweli hasa baada ya kuthibitishwa na waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu aliyeeleza kuwa amepata taarifa kutoka kwa mashuhuda wa ajali hiyo kuwa kuna chopa imeanguka na kulipuka katika eneo la Kitalu R3.

Mapema leo asubuhi, Waziri Nyalandu alieleza kupitia Twitter kuwa ametuma vikosi vya askari wa uokoaji katika eneo hilo la tukio kufanya kazi na kutoa picha halis pamoja na hali za wahanga wa ajali hiyo.

“Maafisa na Maaskari wanaelekea eneo la tukio kutokea Msolwa, na Matambwe, na tumeagiza vikosi vilivyo kwenye doria Selous kushiriki uokoaji,” alitweet Waziri Nyalandu. Mapema leo asubuhi, Nyalandu amesema, “Ndege za uokozi zinatua Uwanja wa ndege wa Msenguni, karibu na Msolwa katika mbuga ya Selous asubuhi ya leo.”

 

 

Ujenzi Wa Barabara Za Juu ‘Flyover’ Kuanza Mwezi Ujao, Magufuli Anena
Simba Yawatakia Watanzania Uchaguzi Mwema