Matatizo ya usafiri katika Gereza la Segerea yamesababisha kutofikishwa mahakamani Mkurugenzi wa mradi wa mabasi yaendayo kasi Dar es salaam (UDART), Robert Kisena (46) na wenzake watatu.

Mbali na kisena, washtakiwa wengine ni kulwa kisena (33), Charles Newe (47), na raia wa China, Cheni Shi (32), ambapo jana ilitakiwa kesi yao itajwe mbele ya hakimu mkazi mkuu, Thomas Simba wa Mahakama ya hakimu mkazi kisutu ili kuangalia kama upelelezi wa kesi yao umekamilika au bado.

Upande wa mashtaka katika kesi hiyo ukiongozwa na wakili wa Serikali, Wankonyo Saimon, ulitoa madai hayo jana wakati shauri hilo lilipotajwa, wakili Wankonyo akadai kuwa washtakiwa hawajafika Mahakamani kwasababu ya tatizo la usafiri wa mahabusu wa gereza la Segerea.

Hata hivyo baada ya maelezo ya wakili huyo, Hakimu Simba aliahirisha kesi hiyo hadi Mei 6, 2019 itakapotajwa tena katika Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu.

Awali upande wa mashtaka ulieleza Mahakama kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika na bado wanasubiri maelekezo kutoka kwa Mkurugenzi wa mashtaka nchini (DPP).

Kisena na wenzake wanakabiliwa na mashtaka 19 likiwemo la utakatishaji wa fedha na kuusababishia mradi wa UDART hasara ya zaidi ya sh bilioni 2.

Katika mashtaka hayo lipo moja la kuongoza uhalifu, kujenga kituo cha mafuta bila kibali, kuuza mafuta sehemu zisizoruhusiwa pamoja na wizi wakiwa wakurugenzi pia wanakabiliwa na mashtaka manne ya kughusi kutoa nyaraka za uongo manne, mashtaka mawili ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kusababishia maradi huo hasara.

Wanajeshi 30 wa Nigeria watoweka
Video: Mwakyembe alinyweshwa sumu, Nataka vyama vingi viendelee - JPM

Comments

comments