Mashetani wekundu (Manchester United) wameonyesha kuwa tayari kumsajili mshambuliaji kutoka nchini Sweden Zlatan Ibrahimovic, aliye huyo kwa sasa, baada ya kumalizana na klabu bingwa nchini Ufaransa PSG mwishoni mwa juma lililopita.

Man Utd wameonyesha utayari wa kumsajili mshambuliaji huyo, kufuatia mipango yaliyonayo kwa sasa ya kutaka kumpa nafasi Jose Mourinho kama mkuu wa benchi la ufundi, kwa kuamini Zlatan ana mahusiano mazuri na mreno huyo.

Taarifa za awali zinaeleza kwamba, Jose Mourinho amepanga kumpeleka Zlatan, Old Trafford na huenda akawa tayari kumlipa mshahara wa Pauni 400,000 kwa juma.

Hata hivyo pesa hizo zimetolewa ufafanuzi wa kina kwa kuelezewa kwamba, kiutaratibu mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 34, atastahili kulipwa mshahara wa Pauni 250,000 lakini atanufaika marupurupu ya Pauni milioni 8, zitakazotokana na ada yake ya usajili ambayo itaingia mfukoni mwake kama mchezaji huru.

Tajiri Wa Paris Saint-Germain Amtengea Fungu La Pesa Ronaldo
FIFa Waendelea Kutumbuana