Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi amefurahishwa na ushirikiwaji wa wazawa katika Mradi wa Reli ya Kisasa, ambao umeweza kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

Katambi ameyasema hayo baada ya kutembelea Mradi wa Reli ya Kisasa – SGR Mkoani Tabora kwa lengo la kukagua utekelezaji wa sheria za kazi na masuala ya afya na usalama mahala pa kazi na kuongeza kuwa asilimia 90 ya manunuzi ya bidhaa na vifaa katika mradi huo yanafanyika kwa lengo la kutunza thamani ya fedha, kuongeza ajira na ukuaji wa uchumi.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi (kushoto) akizungumza na viongozi wa kampuni ya Yapi Markezi alipotembelea Mradi wa Reli ya Kisasa, kwa lengo la kukagua utekelezaji wa sheria za kazi na masuala ya afya na usalama mahala pa kazi, Mkoani Tabora.

Amesema, “niendelee kusisitiza suala la Local Content liendelee kuzingatiwa katika mradi huu. Pia malighafi ambazo si lazima zitoke nje ya nchi ni vyema zikanunuliwa hapa nchini ili kuwawezesha ukuaji wa uchumi wetu.”

Aidha, ameongeza kuwa mpango wa urithishaji wa ujuzi kwa wazawa utekelezwe ipasavyo ili wataalamu wanapomaliza muda wa kufanyakazi hapa nchini, wazawa waweze kufanya kazi hizo badala ya kuwaacha wataalamu hao wa kigeni kuendelea kuomba vibali vya ajira.

Mkuu wa Wilaya ya Tabora, Louis Bura (kulia) akieleza jambo wakati wa ziara hiyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa sheria za kazi na masuala ya afya na usalama mahala pa kazi katika mradi wa Reli ya Kisasa Tabora – Isaka, Mkoani Tabora.

Hata hivyo, Naibu Waziri Katambi amewataka wakandarasi wadogo pamoja na makampuni yanayotoa huduma katika mradi huo kuhakikisha wanatekeleza sheria ya ajira na mahusiano kazini.

Clifford Mario Ndimbo aula tena CAF
Waziri Mkuu ataka ushirikiano utoaji elimu ya fedha kwa vijana