Uwanja wa Ndege wa kijeshi wa Tayfur maarufu kama T4 nchini Syria uliopo karibu na mji wa Homs  umeshambuliwa kwa makombora na kusababisha vifo vya watu.

Taarifa iliyotolewa na vyombo vya habari nchini humo vimesema kuwa mpaka sasa haijafahamika aliyehusika na shambulio hilo, japokuwa hapo awali Marekani ilidhaniwa kuhusika na tukio hilo kutokana na Historia hiyo kujirudia nchini humo.

Aprili, mwaka jana Marekani ilirusha makombora 59 aina ya Tomahawk katika uwanja wa ndege za kivita wa Shayrat nchini Syria baada ya shambulio la kemikali kutekelezwa katika mji wa Khan Sheikhoun uliokuwa unashikiliwa na waasi.

Aidha maafisa wa Marekani wamekanusha kuhusika na tukio hilo, zaidi wamedai kulipiza kisasi dhidi ya tukio la shambulio hilo nchini Syria na wamedai kuwa kwasasa Wizara ya ulinzi haitekelezi mashambulio yeyote ya angani nchini Syria.

“Hata hivyo, tunaendelea kufuatilia kwa karibu na kuunga mkono juhudi za kidiplomasia zinazoendelea za kuwawajibisha wote wanaotumia silaha za kemikali, nchini Syria na kwingineko, kuhakikisha wanaadhibiwa.” imesema Pentagon.

Hata hivyo, Rais wa Marekani, Donald Trump na Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron wameapa kuchukua hatua kali na ya pamoja kuhusiana na shambulio hilo.

Twiga Stars yang'olewa
Magazeti ya nje na ndani ya Tanzania leo Aprili 9, 2018