Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Uholanzi Louis van Gaal amesema kikosi chake hakitafanya ishara yoyote, itakayopingana na taratibu za Fainali za Kombe la Dunia, watakapocheza mchezo wa Pili dhidi ya Ecuador baadae leo Ijumaa (Novemba 25).

Uholanzi imepinga kupanga kufanya mambo tofauti na taratibu za Fainali hizo zinazoendelea nchini QATAR, baada ya Kikosi cha Ujerumani kuonyesha ishara ya kuziba midomo kabla ya mchezo wao wa Kwanza dhidi ya Japan, kwa lengo la kuwasilisha ujumbe wa ‘Kunyamazishwa na FIFA’.

Ishara hiyo ilikuja baada ya FIFA kuwatishia Manahodha wa Timu za Taifa kutoka Barani Ulaya, ambao walipanga kuvaa Kitambaa cha Unahodha chenye ujumbe wa ‘OneLove’ wakati wa Fainali hizo, kwa lengo la kuunga mkoni Mapenzi ya Jinsia Moja.

“Hapana, hatutafanya lolote ambalo linapingana na taratibu zilizowekwa na FIFA, tulisitisha mpango huo mara baada ta FIFA kukataza, tupo hapa kushindana sio kugombana na yoyote,” amesema Van Gaal

Uholanzi ilianza Kampeni ya kusaka taji la Dunia Jumatatu (Novemba 21), kwa kuichapa Senegal 2-0 katika mchezo wa Kwanza wa Kundi A.

TBS yawataka wafanyabiashara kushirikiana na taasisi za serikali
ICC kuthibitisha mashtaka dhidi ya Kony