Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa leo Machi 13, 2018 amesema kuwa uchunguzi uliofanywa na jeshi la polisi kuhusu taarifa za kutekwa kwa Abdul Nondo umedai kuwa mwanafunzi huyo alijiteka mwenyewe.

Amesema hayo mapema hii leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa Nondo alikamatwa huko Mafinga Iringa akiendelea na shughuli zake na kusema hakuripoti sehemu yoyote kuhusu kutekwa kwake.

“Pengine alitaka kuzua hilo ili kujipatia umaarufu ila upelelezi uliendelea kubaini kuwa mwanafunzi huyo alikwenda Iringa kwa mpenzi wake ambaye alikuwa akiwasiliana naye mara kwa mara akiwa njiani kuelekea Iringa hii ni baada ya kufanya uchunguzi wa kisayansi na kubaini muda ule aliosema ametekwa simu yake imeendelea kuonyesha mawasiliano aliyokuwa anafanya na huyo binti ambaye alikuwa amemfuata,”amesema Kamanda Mambosasa

Young Africans waifuata Township Rollers
Wananchi wenye hasira kali wachoma moto gari

Comments

comments