Ali Kiba leo ameachia wimbo mwingine mpya alioupa jina ‘Mwambie Sina’, akiwa na wasanii wapya aliowatambulisha rasmi wiki hii kwenye lebo yake ya ‘Kings Music’.

Ali Kiba anawaongoza Abdu Kiba, Cheed, K2ga na Killy kwenye ngoma hii ya mapenzi ambayo video yake imeongozwa na Hanscana.

Kibwagizo kilichowekwa sawa na Ali Kiba mwenyewe kimetanguliwa na shairi fupi la Killy.

Mashambulizi yanaendelea baada ya kijiti kukipokea Cheed na mwisho Abdu Kiba na Kiba mwenyewe akimalizia; wakijaribu kumtuma mjumbe afikishe ujumbe kwa mrembo.

Video: Dodoma yaibuka kidedea, Mbeya yashika mkia ukusanyaji mapato
Majaji watumbuliwa kwa rushwa

Comments

comments