Baraza la madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma, limeazimia kumrejesha kazini mhandisi wa Halmashauri hiyo, Vivian Mndolwa na kumlipa nusu mshahara kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Hayo yamethibitishwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya hiyo, Ambros Nchimbi ambapo ameeleza kuwa mhandisi huyo alisimamishwa kazi kufuatia kesi ya kinidhamu katika kusimamia mradi wa maji katika kijiji kilichopo wilayani humo, ambapo baada ya uchunguzi alichukuliwa hatua hizo.

Nchimbi amesema Baraza la madiwani lilikaa na kuamua kumpunguzia mshahara kwa nusu ya mshahara wake kwa muda wa miezi 12.

Wachezaji Simba, Yanga wanaotumia dawa kuongeza nguvu kujulikana
Zitto Kabwe: Hatukutaka mnunue ndege hovyo hovyo