Katika michezo ya Ligi Kuu Hispania(La Liga) iliyochezwa usiku wa Septemba 21 2016 mchezo uliovuta hisia za mashabiki wengi ni mchezo kati ya Barcelona dhidi ya Atletico Madrid uliochezwa Nou Camp.

Pamoja na Barcelona kumiliki mpira kwa asilimia 70 katika mchezo huo wameshindwa kutamba baada ya kulazimishwa sare ya goli  1 – 1 na kufuatia matokeo hayo sasa wanakuwa nafasi ya tatu kwa kufikisha jumla ya point 10, wakati Atletico wakiwa nafasi ya pili kwa kuwa na point 11 na Real Madrid wanaongoza Ligi hiyo kwa kuwa na point 13.

Barcelona ndio walikuwa wa kwanza kupata goli dakika ya 41 kupitia kwa Ivan Rakitic ambapo Lionel Messi alitolewa nje dakika ya 51 baada ya kuumia, na baadae Atletico Madrid wakasawazisha dakika ya 61 kupitia kwa Angel Correa.

Lakuvunda Halina Ubani, Kompany Ashindwa Tena
Diego Godin Amkalisha Messi, Kurejea Uwanjani Mwezi Ujao