Katika kuhakikisha kuwa juhudi za serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli zinaungwa mkono.

Kampuni ya Habari ya Dar24 Media imefanya tamasha kubwa Tabata Jijini Dar es salaam la kutoa elimu kuhusu madhara ya dawa za kulevya.

Tamasha hilo limefanyika Tabata Mawenzi Jijini Dar es salaam, likiwa na lengo la kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya Tano ya kuwapa elimu na kuwakomboa vijana kuepukana na wimbi la matumizi ya dawa za kulevya.

Akizungumza katika tamasha hilo linalojulikana kwa ‘SHTUKA’,lenye kauli mbiu yake isemayo “Shtuka Piga vita dawa za kulevya,” Katibu Mkuu wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Methew Lucas Bicco ameipongeza Dar24 Media kwa kuandaa tamasha hilo kwani vijana wengi wamekuwa wakijiingiza katika janga la utumiaji wa dawa za kulevya.

Aanza safari kwa baiskeli kuelekea Urusi kushuhudia kombe la dunia 
Musiba awavaa TEF, awataka kutotumika kisiasa

Comments

comments