Wasanii wa muziki wa Bongo Fleva kutoka katika label ya WCB, Diamond Plutnumz na Rayvanny wameliomba msamaha Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) mara baada ya kufungiwa kushiriki matamasha ya muziki ndani na nje ya nchi kwa muda usiojulikana.

Siku chache zilizopita Baraza la Sanaa Tanzania liliufungia wimbo wa ‘Mwanza’ kutokana na kutokuwa na maadili, BASATA pia walitangaza kulifungia Tamasha la Wasafi Festival na kuwataka wasanii hao kutoshiriki ama kutumbuiza katika nchi nyingine yoyote pamaoja na kwamba walishapanga kwenda kutumbuiza nchini Kenya katika tamasha la Wasafi Festival.

Aidha, wasanii hao wameibuka na kuomba msamaha kwa Baraza la Sanaa Tanzania na Serikali kwa ujumla na kuapa kutorudia tena kosa lililotokea, na kuomba kusamehewa adhabu yao.

 

Video: Kwenye suala la fedha sinaga uvumilivu- JPM
Rais Museveni ampa dongo Miss Uganda

Comments

comments