Waziri wa Habari wa Sanaa Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kuwa amesikitishwa sana na Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) kukosa wanafunzi wa kufundisha Kiswahili.

Ameyasema hayo mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea Ofisi hizo zilizopo jijini Dar es salaam, ambapo amesema kuwa Baraza hilo lina fursa kubwa ya kuweza kukitangaza Kiswahili duniani kote.

“Yaani Baraza la Kiswahili mnakosa wanafunzi wa kiswahili, Baraza hili ndilo lilitakiwa kuwa na takwimu ya balozi zote za Tanzania duniani kote, Tanzania inatakiwa kuwa ni balozi wa Kiswahili duniani kote, nchi zingine ziwe zinakuja kuchukua waalimu wa Kiswahili kutoka Tanzania,”amesema Dkt. Mwakyembe

Aidha, Dkt. Mwakyembe amelitaka baraza hilo kutolala kwani likifanya hivyo litakuwa linaididimiza lugha ya Kiswahili hivyo kupoteza fursa iliyopo ya kufundisha nchi nyingine zenye uhitaji wa kujua lugha ya Kiswahili.

Hakimu Ataka Upelezi Wa Kesi Ya Viongozi Wa Simba Ukamilishwe Haraka
Video: Dkt. Mwakyembe awawashia moto Bima