Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema kuwa kuwekwa kando katika nafasi hiyo hakumfanyi aachane na ubunge.

Dkt. Mwigulu amsema hayo leo Julai 7, 2018 katika mkutano na wananchi wa kijiji cha Misigiri Kata ya Ulemo mkoani Singida ambapo amesema kuwa jambo hilo haliwezi kumfanya aachane na ubunge.

Amewasisitizia kwamba yeye bado ni mbunge na kwa sasa si Waziri tena, huku akijifananisha na mchezaji aliyeachwa na timu yake ya Taifa. “Kwa sasa mimi ni mbunge. Mchezaji akiachwa timu ya Taifa anarudi kuitumikia klabu yake, mimi nimerejea kwenye klabu yangu (ubunge),” amesema.

Hivi karibuni, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amefanya mabadiliko madogo katika baraza la mawaziri ambapo amemtupa nje kiongozi huyo ambaye ni mbunge wa Iramba Magharibi na nafasi yake ikachukuliwa na Kangi Lugola.

Rais Magufuli kuipokea ndege mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner
JPM awatunuku kamisheni maofisa 118 wa Jeshi la Wananchi (JWTZ)

Comments

comments