Nyota mpya anayeng’ara kwenye anga ya Bongo Flava, Foby amefunguka yanamhusu akiwaweka kwenye sentensi zake, Diamond, Ali Kiba na malkia wa muziki huo nchini, Lady Jay Dee.

Mkali huyo wa ‘Star’ na ‘Ila’ amesema amefunguka katika mahojiano aliyofanya na Dar24 hivi karibuni, ambapo ameeleza kuhusu safari yake ya muziki, utunzi wa nyimbo zake pamoja na namna anavyoweza kuwaandikia mashairi wasanii wengine.

Tofauti na wasanii wengi, Foby ambaye amedai kuwa amekuwa akiandika ngoma nyingi za wasanii wakubwa licha ya kutopewa haki ya sifa stahiki, hivi sasa ameamua kuwa kwa kila wimbo mmoja anaoandika atalipwa shilingi laki tano.

Katika hatua nyingine, msanii huyo amezungumzia kile ambacho baadhi wamekuwa wakikizungumza kutaka kumfananisha na mafahari wa Bongo Flava, Ali Kiba na Diamond huku akimtaja Lady Jay Dee kwenye hoja ya mwanamuziki wa kike anayemkubali zaidi.

Usikose kuiangalia video hii, upate kile usichopaswa kukikosa:

Rais wa TFF atuma salamu za rambirambi Simba
Eminem ajipanga kuwafuta machozi waathirika ugaidi Manchester