Mwenyekiti wa chama cha CHAUMA, Hashim Rungwe amewataka Watanzania kuwa na umoja na mshikamano ili waweze kufikia malengo yao.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na Dar24 Media ambapo amesema kuwa katika nchi yeyote inayotaka kupiga hatua za maendeleo ni lazima kuwa na umoja na mshikamano.

“Sisi tunafuata tu jinsi viongozi wanavyotaka wao, na hawa viongozi wa sasa wana mawazo yao, na wakija wengine watakuwa na mawazo yao, nasema hivyo kwasababu wale walioko madarakani hawataki kupata ushauri wa aina yeyote,”amesema Hashim Rungwe

Video: Matibabu ya Lissu yawaumbua Chadema bungeni, Mtifuano wabunge Makonda
Video: ZOOM Tanzania, Brightermonday wafungua milango kwa wahitimu wa vyuo vikuu