Msanii wa muziki wa Bongo fleva, Rayvanny ameachia video ya wimbo wake unaokwenda kwa jina la ‘Zezeta’.

Kabla haajaachia video hiyo, hivi karibuni wakati akitambulisha ujio wake alimshukuru Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ kwa kuwa ameshiriki kwa kiasi kikubwa katika video yake kwa kumpa ushauri jinsi ya kufanya video hiyo mara baada ya kumtumia wimbo, ndipo alipomshirikisha na director Erick Mzava na kuanza kushoot.

“Ni mtu poa sana, ni mtu ambaye alijiweka mbele kwenye suala la kijana wake, ninakumbuka hata tulipoenda kushoot mambo ya location yeye ndiye alikuwa anapangilia utafikiri video yake” amesema. Tazama hapa video

Bendera aitaka TADB kuwekeza mkoani Manyara
Video: Mapya yaibuka ajali iliyoua wanafunzi 33, Mvua yaliza wabunge