Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa Taifa Stars, inahitaji kupewa pongezi licha ya kupoteza kwa bao 2-0 dhidi ya Senegal, kwenye mchezo wake wa kwanza kwenye michuano ya AFCON inayoendelea nchini Misri.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam, wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa ghala la taifa la mitambo ya gesi nchini, ambapo amesema kuwa wachezaji hao wa Taifa stars walijitahidi katika mchezo huo.

“Kwenye uwanja wa mpira kuna kushinda na kushindwa kwa hiyo wao wakazane, wajitume zaidi na sisi tuendelee kuwaombea, mimi nina uhakika hata huo mwanzo sio mbaya sana, kufungwa magoli mawili tu na timu ambayo inaongoza Afrika sio jambo baya, tuendelee kuwapa moyo” amesema Rais Magufuli.

Kwa upande wake, Mkuu Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema kuwa anaumizwa sana na tabia ya baadhi ya watu kupitia mitandao ya kijamii kuonyesha kuwabeza wachezaji wa timu ya taifa.

“Nilikuwa natamani kuomba kibali angalau niende tu kule kambini lakini ikikupendeza Mh. Rais utajua mwenyewe utakavyoamua. Najisikia faraja vyombo vyote kule vinatangaza habari ya Tanzania, leo tunasema hawana lolote, hawana lishe, maneno haya ya kukatisha tamaa hayana tija” amesema Makonda

LIVE: Yanayojiri Bungeni jijini Dodoma leo Juni 26, 2019
Video: Bahati mbaya huyu kijana wetu hajitambui, anapeleka uongo kwa JPM- Ndugai

Comments

comments