Jumuiya ya Umoja wa Vijana UVCCM, UDSM wamepongeza hatua mbalimbali za kimaendeleo zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuweza kununua Ndege na kutoa elimu bure.

Wametoa pongezi hizo jijini Dar es salaam walipokuwa wakizungumza na waandishi wa habari, ambapo wamesema kuwa hakuna haja ya kupinga maendeleo hayo ambayo yanaifanya nchi kupiga hatua za kiuchumi.

Wamesema kuwa katika kipindi cha miaka mitatu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, kuna mabadiliko makubwa ya kimaendeleo, hivyo wamewaasa wananchi kuendelea kuunga mkono juhudi hizo.

”Sisi tunawaomba wananchi waendelee kumuunga mkono rais wa wanyonge, John Magufuli kwa juhudi zake za kuliletea maendeleo taifa letu,” Wamesema UVCCM

Video: Mahojiano ya Lissu, BBC yalivyotikisa dunia haya hapa
Mnyeti aruhusu wanaApolo kuingia bure kwenye ukuta wa JPM

Comments

comments