Msanii maarufu hapa nchini, Muhogo Mchungu amesema kuwa kwa mara ya mwisho kuongea na marehemu King Majuto alimwambia kuwa anataka kurudi kuishi shamba.

Muhogo ameyasema hayo jijini Dar es salam alipokuwa akizungumza na Dar24 Media, ambapo amesema kuwa King Majuto alisema maneno hayo alipokwenda kumjulia hali katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

“Kwa mara ya mwisho, King Majuto aliniambia anataka arudi kuishi shamba, na mimi nikamjibu kiutani nikamwambia nimekulia mjini tangu kijana leo hii uzeeni nikafanyeje shamba, tukabaki wote tunacheka tu,”amesema Muhogo Mchungu

 

Salah, Ronaldo, Messi kuwania tuzo Ulaya
Video: Hali ilivyokuwa baada ya JPM na Kikwete kukutana kwenye msiba wa 'King Majuto'

Comments

comments