Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Magdalena Sakaya amewataka wanachama wa chama hicho kushikamana na kuweza kukiimarisha chama hicho.

Ameyasema hayo hii leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa mgogoro uliokuwa unakisumbua chama hicho umemalizika hivyo kwa sasa kazi iliyobaki ni kuunganisha nguvu.

Amesema kuwa kesi iliyokuwa mahakamani imeshamalizika hivyo kazi kubwa iliyobaki kwa sasa ni kuondoa tofauti zilizokuwepo ili kuanza kukijenga chama hicho upya kwaajili ya maandalizi ya uchaguzi.

”Kwa sasa niwaagize viongozi wote wa chama walioko katika ngazi zote kuanza kufanya kazi kwa pamoja na mshikamano na wanachama, kwani kwa sasa tumeshamaliza kesi yetu, hivyo hela zilizokuwa zimezuiliwa kwenye akaunti tumeruhusiwa kuzitumia,”amesema Sakaya

Kibaha wailalamikia Kampuni inayojenga stendi mpya
Okwi aweka historia Taifa wakati Simba ikiiangamiza Ruvu Shooting