Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema kuwa idadi ya watu wanaohitaji kusaidiwa migiuu ya bandia imeongezeka hadi kufikia 1000, hivyo amewaasa wananchi wenye mapenzi mema kujitokeza na kuchangia walichonacho.

Ameyasema hayo jijijni Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema idadi hiyo imeongezeka mara baada ya watu kutoka mikoa mbalimbali kuonyesha uhitaji wa hali ya juu.

”Idadi ya watu inazidi kuongezeka kwakuwa wanatoka mikoa mbalimbali hivyo hatuna budi kuwahudumia kwakuwa wanahitaji kuendelea na shughuli zao, hivyo niwaombe wananchi wa Dar es salaam wajitokeze kujitolea kuwasaidia ndugu zetu,”amesema Makonda.

Hata hivyo, Makonda amewashukuru wadau mbalimbali ambao wanaendelea kujitokeza kwaajili ya kutoa misaada itakayowawezesha wananchi hao wenye uhitaji wa miguu hiyo ya bandia

Magazeti ya Tanzania leo Agosti 22, 2017
NEC yateuwa Madiwani 12 wanawake wa viti maalum