Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amemjibu Mkurugenzi wa CZI, Cyprian Musiba kwa kumtuhumu kuwa ni mtu hatari kwa usalama wa taifa.

Ameyasema hayo mapema hii leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa tuhuma hizo si za kweli.

Amesema kuwa shutuma hizo si za kweli bali ametumwa na watu wasiowatakiwa mema katika kuliletea maendeleo taifa.

“Huyu Musiba ametumwa, yale maneno amerishwa kwa makusudi ili kuandaa mazingira ya kutukamata, anasema tumefundisha vijana 400 kwa ajili ya kufanya vurugu, hii si kweli,”amesema Mbowe

Mke wa Mugabe kikaangoni sakata la ‘PhD feki’, mwalimu wake akamatwa
Video: Musiba kuburuzwa kortini