Mgombea wa wa kiti cha ubunge wa Chama cha Wananchi (CUF) Jimbo la Kinondoni, Rajabu Salum Juma amesema kuwa yeye anamuunga mkono Rais Dkt. John Magufuli lakini hawezi kukihama chama hicho.

Amesema kuwa kuachia jimbo na kwenda kumuunga mkono rais, huku ukisababisha kurudiwa kwa uchaguzi ambao unagharimu fedha nyingi si jambo la kiungwana.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na Dar24 Media, ambapo amesema kuwa kufanya hivyo si dhambi kwani unaweza kumuunga mkono ukiwa ndani ya chama chako na si mpaka ukaungane nae kwenye chama chake.

“Kumuunga mkono mtu si lazima uwe kwenye chama chake, kwa mfano mimi namuunga mkono rais Dkt. John Magufuli lakini siwezi kukihama chama changu,”amesema Juma

Hata hivyo, ameongeza kuwa kama wananchi wa Kinondoni wakimchagua basi atahakikisha kuwa baadhi ya mahitaji muhimu yanapatikana kwa wakati

Manara awaonya mashabiki wa Simba kuhusu Yanga
Magereza yaeleza sababu za kumzuia Profesa Jay kumuona Sugu gerezani

Comments

comments