Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu Cha Dar es salaam (UDSM), Prof. Alexander Makulilo amesema kuwa siasa ni afya hivyo watu wote hawawezi kuwa na itikadi moja.

Ameyasema hayo Jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na Dar24 Media ambapo amesema kuwa watu wanapokuwa na itikadi tofauti huzalisha fikra mpya ambazo huwa ni kichocheo cha maendeleo.

Amesema kuwa siasa imekuwa ikibadirika kulingana na mazingira husika, kwani ukilinganisha tangu nchi ipate uhuru mpaka leo kuna mabadiliko makubwa.

“Sitarajii hata siku moja kwamba watu wote tutakuwa na fikra moja, kwasababu itikadi tofauti ni afya ya akili, kwani husababisha kuibua fikra mpya,”amesema Prof. Makulilo

Magazeti ya Tanzania Aprili 6, 2018
Kesi ya Aveva na mwenzake yakwama, warudishwa Gerezani

Comments

comments