Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Jenista Mhagama amesema kuwa Serikali imepata ukakasi mara baada ya kupata taarifa za mwalimu aliyewadharirisha wanafunzi wa kike wa shule ya Mt. Florence iliyopo jijini Dar es salaam.

Amesema kuwa tayari Serikali imeagiza Idara husika kuchukua hatua mara moja dhidi ya Mwalimu aliyefanya kitendo hicho kwani ni udharirishaji mkubwa.

Ameyasema hayo Jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na Dar24 Media ambapo amesema kuwa Wizara husika imeshaanza kuchukua hatua ili Serikali iweze kutoa taarifa sahihi.

“Pamoja na ukakasi huu tunaomba tupewe nafasi ya kulifanyia kazi suala hili ili tuweze kuja kutoa majibu ambayo yako sahihi, kwani kwasasa Idara husika zimeshaanza kulifanyia kazi,”amesema Mhagama

Magazeti ya Tanzania leo Juni 2, 2018
Video: Dkt. Hellen Kijo-Bisimba akanusha kuteuliwa baraza la wazee Chadema