
Baada ya subira ya muda mrefu ya mashabiki wa muziki wa bongo fleva, Barakah Da Prince ameachia rasmi video mpya ya wimbo wake ‘Nisamehe’ aliomshirikisha Ali Kiba.
Video hiyo inayowakutanisha kwa mara ya kwanza wasanii hao wa Rock Star 4000 imepikwa nchini Afrika Kusini na kuongozwa na Meji Alabi.