Mariam Manyama, aliyeongoza kitaifa katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne, amesimulia jinsi alivyowahi kuanguka na kupata alama ambazo haziridhishi akiwa kidato cha tatu.

Msichana huyo ameeleza kuwa aliwahi kupata daraja ‘C’ katika moja ya mitihani yake ya kidato cha tatu, na aliamua kujiadhibu mwenyewe mbali na adhabu aliyopewa na walimu wake.

Msikilize hapa kwenye mahojiano maalum na Dar24, upate undani wa simulizi lake zuri la kupanda, kushuka na kumaliza akiwa kwenye kilele cha mafanikio ya elimu ya kidato cha nne. Pia, ameeleza shule anayopenda kusoma na changamoto anazoziona mbele yake.

Bundi atua ndani ya Bunge, Spika Ndugai awatoa hofu wabunge
Majaji walalama ukata, wamuomba Rais aingilie kati