Mtoto Ibrahim Hassan anayeishi Kigamboni Jijini Dar es salaam amepata na ugonjwa usiojulikana ambapo alidondoka ghafla akiwa shuleni.

Akizungumza na Dar24 Media, Mama wa kijana huyo, Fatuma Mohamed amewaomba Watanzania kumsaidia ili aweze kumpeleka mtoto huyo katika hospitali ya taifa Muhimbili.

Amesema kuwa mwanae huyo ana ndoto za kusoma na kufika mbali hivyo anahitaji msaada wa haraka ili aweze kumpeleka hospitali.

“Nawaomba Watanzania wanisaidie, mtoto wangu alianguka tu ghafla akiwa shuleni, ninaomba sana msaada wa fedha za kumpeleka hospitali,”amesema Mama wa kijana huyo Fatuma Mohamedi

Wizara yatoa ufafanuzi juu ya kitabu kilichokosewa kuchapishwa
Mabasi ya mwendokasi yasitisha safari baadhi ya maeneo Dar

Comments

comments