Msanii wa muziki wa Bongo, Nay wa Mitego siku chache zilizopita ameachia ngoma yake mpya inayoitwa ‘Alisema’ ambapo ngoma hiyo amezungumzia hali ya kimaisha hapa nchini.

Kiitikio cha wimbo huo kimenirudisha nyuma enzi za mchakamchaka na enzi zile za Nyerere, Ney ameimba ”Alisema mwalimu tuamke na sasa tuanze mchakamchaka” ni sauti ya kidijitali iliyotumika inavutia kutaka kuendelea kusikiliza wimbo huo na kujua ni mashairi gani yatatajwa.

Mbali na kusifia makubwa aliyofanya Mhe. Rais Joh Pombe Magufuli kuna mambo kadhaa Ney amehoji juu ya hatma ya watanzania hususani engo ya vyombo vya habari, maisha ya watanzania kwa ujumla, kifo cha mtoto Akwilina na kadhalika.

Moja ya mistari katika wimbo huo Ney ameimba ”Naona hofu imetanda watu wanaogopa kusema, maisha yamekuwa magumu nayo mnaogopa kusema, acheni uoga mkihisi mtakufa mapema, Rest in Peace Akwilina Mungu akulaze pema kesi ya kifo chako huku bado ni lawama”.

Wimbo huu Ney amecheza salama tofauti na tulivyomzoea katika nyimbo zake za nyuma ambazo nyingi zilikuwa zikifungiwa, katika Alisema kihabari tunasema amebalance stori.

Ni wimbo mzuri wa kusikiliza na kujifunza kwani unahamasisha vijana kufanya kazi, viongozi kutekeleza majukumu yao.

Utizame na sikiliza neno kwa neno hapa chini.

Huddah amtaka Kenyetta ahalalishe bangi
Nafasi 10 za ajira kutoka makampuni 10 Tanzania

Comments

comments