Timu ya Ngorongoro Heroes imeingia kambini kwa ajili ya kujiandaa na mchezo dhidi ya timu ya Mali inayotarajiwa kuchezwa tarehe 13 mwezi huu katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

Hayo yamesemwa na Afisa Habari wa Shirikisho la Soka nchini Tanzania (TFF), Clifford Mario Ndimbo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi.

“Niwaombe Watanzania wajitokeze kwa wingi kuishangilia timu yetu ili iweze kufanya vizuri katika mashindano haya, tutimize ndoto zetu za muda mrefu,”amesema Ndimbo

Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Mei 3, 2018
Kanye West awakera Wamarekani weusi