Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amewataka Askari Magereza kufanyakazi kwa bidii na kuipenda kazi yao

Ameyasema hayo jijini Mwanza mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika gereza hilo na kuweza kuzungumza na wafungwa pamoja na mahabusu ambapo amewahakikishia kwamba serikali haijawasahau na ina wathamini kama majeshi mengine.

Amesema kuwa jeshi hilo haliwezi kufanyakazi kwa mateso wakati yeye yupo hivyo amewataka kila mmoja ahakikishe anatimiza wajibu wake kwa kuwasimamia vizuri wafungwa na mahabusu.

Aidha, Rais Magufuli amelitaka jeshi hilo kuhakikisha Wafungwa na Mahabusu hawaingii Gerezani na aina yeyote ya silaha au simu kwani vitu hivyo haviruhusiwi kisheria.

”Askari mtambue kuwa hawa watu ni watu wa Mungu, na hii kazi yenu mtambue kuwa ni wito, msiichukie hii kazi mkaona ninyi mko tofauti na majeshi mengine, nimeona kero yenu, nitajaribu kutafta gari ili nilete hapa gereza la Butimba,”amesema Rais Magufuli

Dkt. Kolimba aendesha harambee kuchangia Ujenzi wa Kanisa Njombe
Irene Uwoya awaomba radhi waandishi wa habari, 'Mnisamehe sana'