Wananchi jijini Dar es Salaam wamempongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuzindua rasmi sensa ya watu na makazi itakayofanyika mwaka 2022.

Wakizungumza na kituo cha habari cha Dar 24 Media wameeleza kuwa Rais Samia amefanya uamuzi sahihi kuhusu sensa na itasaidia kutatua changamoto mbalimbali za kijamii.

“Huwezi kutambua mahitaji, namna gani unaweza kusaidia huduma za kijamii kama hautakuwa na idadi ya watu wa eneo husika.” Amesema mmoja wa Wananchi hao.

Aidha wameeleza kuwa sensa husaidia kuinua maendeleo ndani ya Taifa ambapo wamezishauri asasi za kiraia kushirikiana na serikali ili kurahisisha zoezi la sensa.

Hii itakuwa ni awamu ya sita ya sensa ya watu na makazi ambayo imefanywa katika vipindi tofauti tofauti baada ya uhuru 1961, Imefanyika mwaka 1967,1978, 1988, 2002 na 2012

Tatizo la mafuta sasa basi - Majaliwa
Mahakama yamwachia huru Rugemalira