Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli ameondoka nchini leo kuelekea nchini Uganda ambapo anatarajiwa kushiriki mkutano wa 19 wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) utakaofanyika Ijumaa mjini Kampala.

Rais Magufuli ameondoka nchini mapema leo ambapo akiwa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere alisindikizwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda na kuagwa na baadhi ya viongozi akiwemo mkuu wa majeshi ya ulinzi Jenerali Venance Mabeyo.

Lema atajwa kuwa chanzo cha madiwani kuhama chama
Uganda hatarini kukatiwa misaada na UNHCR