Rais Yoweri Museveni wa Uganda ameahidi kujenga vyumba vya madarasa saba katika kijiji cha Nyabirezi kilichopo wilayani Chato mkoa wa Geita mara baada ya kufurahishwa na mapokezi ya wanakijiji wa kijiji hicho.

Ametoa ahadi hiyo wilayani Chato mkoa wa Geita mara baada ya kumaliza ziara yake binafsi ya siku moja, ambapo amesema kuwa amefurahishwa na ukarimu wa wananchi hao ambao wamejitokeza kuwa wingi kumpokea.

”Nimefurahishwa sana na mapokezi mimi nitajenga madarasa saba pindi tu nitakapoonyeshwa eneo la kujenga,”amesema Rais Museveni

Aidha, rais Museveni aliwasilisili hapa nchini hii leo kwa ziara binafsi ya siku moja na kupokelewa na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ambapo amemaliza ziara yake na kurejea nchini Uganda.

 

 

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Julai 14, 2019
Prof. Mbarawa amkataa mhandisi. 'Kashatupiga pesa nyingi sana huyu'

Comments

comments